Gwajima: Nitaendelea Kusema Ukweli Fitina Kwangu Mwiko
Dar es Salaam. Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema ataendelea kusema ukweli na hataogopa chochote.
“Nitaendelea kusema ukweli fitina kwangu mwiko” alisema hayo katika mahubiri yake ya leo kanisani kwake Ubungo.
Pamoja na mambo mengine, Askofu huyo, alisema Clouds Media ni rafiki zake kwa sababu wamewaeleza ukweli watanzania.
Alisema hata waislamu ni rafiki zake kwani ndiyo waliomlea baada ya kutelekezwa akiwa mdogo.
Wasanii maarufu wa redio ya EFM, Mkude Simba na Stanley walikuwa kanisani hapo leo huku Mchungaji Gwajima akiongoza misa kwa mada ya vipaji na vipawa.