-->

Hakuna Haja ya Korabo na Wanaijeria – JB

jacob-Steven-Wema-532

Jb akiwa na Wema Sepetu katika moja picha za filamu ya Chungu cha tatu

MWIGIZAJI mkongwe katika tasnia ya filamu Bongo Jacob Stephen ‘JB’ amesema kuwa haoni sababu ya kuigiza filamu kwa kuwashirikisha wasanii wakubwa kutoka Naijeria au Ghana ili kupata sinema kubwa bali ni kutumia kampuni kubwa za filamu kutoka afrika ya Kusini kufanya nao kazi.

“Hakuna haja ya kuwashirikisha wasanii kutoka Naijeria au Ghana ili kufanya filamu kubwa, Marehemu Kanumba alifanya hivyo kwa wakati ule ilikuwa ni wakati wake, sasa watu wanataka sinema kubwa kutoka kwetu,”JB

Aidha amesema kuwa anathamini mchango wa marehemu Kanumba kuitangaza filamu nje lakini toka kuondoka kwake hakuna aliyefanikiwa kufanya vizuri kuwashirikisha wasanii kutoka nje kwani alikuja Van Vicker kucheza filamu ya Never give up na Hashim Kambi na haikuwa filamu kubwa, JB anaamini kuwa filamu kubwa itatengenzwa na Jerusalem company.

FC

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364