-->

Dotnata, Pacha Wake Majanga

IMG-20160118-WA0001
Staa mkongwe kwenye sinema za Bongo, Illuminata Poshi ‘Dotnata’ akiingizwa kwenye gari la wagonjwa.

DAR ES SALAAM: Staa mkongwe kwenye sinema za Bongo, Illuminata Poshi ‘Dotnata’ na pacha wake, Dometria Alphonce wapo hoi kufuatia mmoja kuanguka bafuni na kuvunjika mfupa wa mguu, mwingine kuvamiwa na majambazi.

Chanzo makini kililiambia gazeti hili juzi kuwa, Dotnata aliteleza bafuni nyumbani kwake River Side jijini Dar na muda huohuo pacha wake huyo akivamiwa na majambazi na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili.index

….Akishushwa kutoka kwenye gari kuingizwa hospitalini.

“Dah! Nahisi kuna kitu, kwa sababu Dotnata ameanguka bafuni na kuumia mguu. Ilikuwa saa kumi jioni, muda huohuo pacha wake akavamiwa na majambazi kule Ukonga-Mazizini, Dar.

Baada ya kupata habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Dotnata kwa njia ya simu ambapo alikuwa na haya:

IMG-20160118-WA0002

Pacha wa Dotnata akiwa amevimba uso.

“Ni kweli niliteleza bafuni na kuanguka. Ni Jumamosi iliyopita, saa kumi jioni. Nimeumia, mfupa wa kwenye paja umevunjika hivyo bado niko Hospitali ya Taifa Muhimbili kwenye kitengo cha mifupa na mishipa ya fahamu (Moi). Jumanne ijayo (juzi) nitafanyiwa operesheni.

“Wakati naanguka, pacha wangu naye alivamiwa na majambazi, wakamjeruhi sehemu mbalimbali za mwili. Alikimbizwa Hospitali ya Hindu Mandal lakini yeye ameshatoka, anaendelea vizuri kidogo,” alisema Dotnata.

 Chanzo: GPL

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364