Hamisa Amlipua Lulu
Mwanamitindo ambaye pia ni video queen maarufu Bongo, Hamisa Hassan Mobeto, amemlipua laivu staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kisa kikidaiwa ni lile saga la kugombea penzi la kigogo (jina tunalo) ambapo kwa sasa hali ni tete baina ya wawili hao.
Hivi karibuni kuliibuka vita kali ya matusi mitandaoni kati ya kundi la mashabiki wa Hamisa linalojiita Team Hamisa na lile la Team Lulu ambapo kila kundi lilitaka kuibuka mshindi huku mada kuu ikiwa ni penzi la jamaa huyo.
Wakati hali ikiwa hivyo, ilibidi wawili hao nao kuvunja ukimya na kuanza kujibizana maneno ya nguoni ambayo yalizua taharuki upya kwa kila upande.
Baada ya kushuhudia malumbano hayo huku kukiwa na maelezo kuwa wawili hao wanachonganishwa, Wikienda lilimtafuta rafiki wa karibu wa Hamisa ili kuanika kiunaga ubaga hasira alizokuwa nazo Hamisa ndipo aliamua kufunguka kwa kumpa makavu Lulu. Mtu huyo alisema kuwa maneno aliyoyatumia Hamisa yalitokana na hasira na hayaandikiki gazetini huku akifafanua kuwa yeye ana mtoto lakini Lulu hana uchungu kwa kuwa bado hajazaa.
Baada ya kujazwa data hizo, Wikienda lilianza kwa kumtafuta Hamisa ili kupata ufafanuzi juu ya sakata hilo ambapo alisema kuwa utaratibu aliojipangia kwenye maisha yake ya siku hizi ni kutotoa taarifa zake kwa waandishi wa habari hivyo asingependa ‘ku-coment’ lolote juu ya hilo japokuwa kila suala lipo wazi.
“Kusema kweli maisha ya sasa kuna muda unaweza kujikuta ukiingizwa kwenye ugomvi ambao hukutarajia na hivyo kwa kuzingatia hilo nisingependa kuongelea tena habari hii maana utaratibu wangu ni kutotoa taarifa wala mambo yangu kuyaweka wazi kwenye magazeti ila kilichoonekana ndicho hicho kwa sasa sina coment yoyote,” alisema Hamisa.
Kwa upande wake Lulu alijibu mapigo kwa kuandika waraka mrefu bila kumtaja Hamisa lakini wapenda ubuyu wakatafsiri kuwa ujumbe umefika. Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na mgogoro kati ya Hamisa na Lulu huku madai ya msingi yakiwa ni kitendo cha Lulu kumchukulia Hamisa baba mtoto wake.
Chanzo:GPL
NUNUA FILAMU KUTOKA STEPS ENTERTAINMENT: TUNAKUFIKISHIA POPOTE PALE ULIPO:
Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.
KAMA UNATAKA KUWA WAKALA WA KUSAMBAZA FILAMU POPOTE PALE:
Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.
Filamu Zilizotoka Hivi Sasa >>>>HIZI HAPA