-->

Mike: Nitakodi Ndege Kupeleka Mahari ya Mrithi wa Thea

Mwigizaji wa kiume Bongo, Michael Sangu ‘Mike’ amesema kuwa anatarajia kukodi ndege kwa ajili ya kwenda mkoani Mbeya kupeleka mahari ya mchumba’ke wa sasa aliyemtaja kwa jina moja la Eliza ambaye ndiye mrithi wa aliyekuwa mkewe, Salome Urassa ‘Thea’.

thea na mike sanga

Akizungumza na Wikienda, Mike alisema kuwa amekuwa akichafuliwa kwa mchumba’ke huyo na watu wanaomwambia maneno lakini wanasahau kuwa huyo ni mpenzi wake wa kitambo hata kabla ya kukutana na Thea.

“Wanaochonga wamechelewa, sasa hivi tumeshafika mbali na nina mpango wa kukodi ndege kwa ajili ya kupeleka mahari kwao (Mbeya) kwani ndiye chaguo langu la mwisho,” alisema Mike.
Mike alifunga ndoa na mwigizaji ‘Thea’ ambaye walitengana kutokana na migogoro ya kindoa, hivi karibuni walidaiwa kupeana talaka.

Chanzo:GPL

NUNUA FILAMU KUTOKA STEPS ENTERTAINMENT: TUNAKUFIKISHIA POPOTE PALE ULIPO:

Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.

KAMA UNATAKA KUWA WAKALA WA KUSAMBAZA FILAMU POPOTE PALE:

Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.

Filamu Zilizotoka Hivi Sasa >>>>HIZI HAPA

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364