-->

Harmonize: Nitafanya Kazi na Ali Kiba Bila Vikwazo

LICHA ya tetesi kwamba wasanii wawili wa muziki wa Bongo Fleva, Ali Kiba na Nasibu Abdul ‘Diamond’, kutoonyesha nia ya kushirikiana katika muziki wao, msanii anayetamba na wimbo wa ‘Bado’, Rajabu Ibrahimu ‘Harmonize’, amesema yupo tayari kufanya kazi na Ali Kiba bila kikwazo chochote.

harmonize-1

Msanii huyo alisema Ali Kiba ni msanii wa Tanzania na ni msanii mzuri katika muziki hivyo kufanya naye ‘kolabo’ ni kitu cha kawaida kama wasanii wengine anavyofanya nao.

“Mimi sijui kiukweli kama kuna bifu kati ya Diamond na Ali Kiba kwa sababu sijawahi kumsikia Diamond akimzungumzia Ali Kiba kwamba wana ugomvi,” alisema Harmonize.

Harmonize ambaye hivi karibuni alijinadi kutoanzisha uhusiano wa kimapenzi, anazidi kujizolea umaarufu kutokana na nyimbo zake tatu ukiwemo ‘Aiyola’, ‘Kidonda Changu’ na ‘Bado’ huku akizidi kujipanga kwa mambo mengine makubwa yatakayokuja kupitia kampuni ya wasafi anayoifanyia kazi.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364