-->

Hawa wa Nitarejea ya Diamond Ataka Menejimenti

Msanii Hawa ambaye alifanya poa kwenye moja ya collabo iliyotikisa Afrika Mashariki, Nitarejea ya Diamond, amefungukia suala la kupata uongozi na kumsimamia kazi zake za muziki.

HAWA DIAMOND

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na east Africa Radio, Hawa amesema anaogopa kutangaza kuwa anahitaji mtu wa kumsimamia (manager) kutokana na aliyoyapitia siku za nyuma, na kuhofia kudharauliwa iwapo atatangaza kuhitaji meneja.

“Naogopa sasa hivi naogopa watu, nahitaji mtu wa kunisimamia, nahitaji kabisaa mtu wa kunisimamia niweze kufanya vitu vyangu, lakini siwezi kujieleza yaani , nikijieleza kwa kila mtu siwezi kumaliza, mtu mwenye imani yake anaweza akanisaidia, lakini siwezi kusema kwa kila mtu naonekana mi mwendawazimu, naonekana kama nimepagawa saa nyingine”, alisema Hawa.

Hawa ambaye siku za nyuma alikumbwa na mikasa tofauti tofauti ikiwemo ule wa kutelekezwa na mwanaume aliyemzalisha, baada ya kutangaza atamsadia na kuishia kumpachika ujauzito.

Kwa sasa mwanadada huyo anaendelea na shughuli za muziki na anaimba muziki wa injili, ingawa bado anaendelea na bongo fleva pia.

Tazama hapa moja ya kazi zake alizofanya hivi karibuni.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364