-->

Hemed PHD: Sitaacha Kujipodoa kwa Hofu ya Watu

MWIGIZAJI wa filamu na msanii wa Bongo Fleva, Hemed Suleiman ‘Hemedy PhD’, amesema kwamba hataacha kutumia vipodozi kwa kuwa humuweka nadhifu na humwongezea mvuto wa mwili wake.

hemed phd

Hemed anayetamba na wimbo wake wa ‘Imebaki stori’, alisema vipodozi anavyotumia zaidi ni poda, lipshine na pafyum na hataacha kujiremba.

“Sitaacha kujiremba kwa sababu kujiremba siyo kwa wasichana tu hata wanaume tunatakiwa tujipake vipodozi, kama poda na lipshine zinasaidia kuongeza mvuto na mwonekano nadhifu zaidi, mimi ni staa natakiwa niishi kistaa hivyo vipodozi ni kitu cha kawaida.

“Mara nyingi vipodozi navitumia nikiwa katika kazi zangu ili nionekane tofauti nyumbani na kazini hivyo nasisitiza kwamba siwezi kuacha kupaka vipodozi kwa kuogopa maneno ya watu,” alimaliza Hemed.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364