-->

Hii Ndiyo Mipango ya Diamond kwa Mwaka Huu

Pamoja na kuwa tumekuwa tukimshuhudia Diamond Platnumz akitangaza kolabo na wasanii wa kutoka Marekani lakini hakuna hata moja tuliyoona hata cover yake,mwaka jana rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete alimuunganisha Diamond na meneja wa Trey Song na ikasema kuwa kuna kolabo itafuta hiyo ni mbali na Swizz Beats,Alicia Keys,Alaine,Kanye West na wengine,na hivi karibuni tumeona picha ya Diamond akiwa na Awilo Longomba inawezekana kuna kolabo itafuata,sasa isue hua inaishia kwenye kupiga picha peke yake au inakuaje?

diamond722

‘’Kuna kitu ‘sometimes’ tunasema wanamuziki wenzangu wa Tanzania tusikimbilie katika soko ikiwa kuna soko ambalo hatujalimaliza kwahiyo napiga hapa katikati kolabo nyingi za Waafrika ili niishike Afrika na nijizatiti zaidi usisahau kama mimi sijaanza ‘tour’ yangu rasmi Afrika bado kwasababu nishaona wanigeria wakipiga ‘tour’zao Gabon na sehemu zingine ,na ndio ‘target’ yangu kwa mwaka huu’’ Alisema Diamond.

‘’Na sio kwamba nilikuwa sipati ‘tour’ lakini nilikuwa sitaki kufanya shoo kiudogo ya watu elfu kumi kwenye ‘viklabu’ unaenda Ghana unapiga shoo klabu ni kujidharirisha watu wanakuona unaenda huko wanategemea upige uwanjani’’ Aliongeza Diamond.

cloudsfm.com

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364