-->

Dudu Baya Amuomba Radhi Shetta

Msanii Dudu baya ambaye alikuwa na ugomvi na msanii mwenzake Sheta, na kumtolea maneno machafu kwenye kipande cha video kilichosambaa kwenye mitandao ya kijamii, amemuomba msamaha msanii huyo na kumtaka kuwe na amani kati yao.

dudu baya23

Kwenye ukurasa wake wa instagram Dudu Baya amepost picha ya Sheta huku akiandika ujumbe mrefu wa kumuomba radhi msanii huyo.

“Habari zenu mashabiki zangu? Ningependa kuchukua nafasi hii leo maalumu kwa ajili ya kukuomba samahani mdogo wangu Nurdin Bilal (Sheta) kwa ajili maneno machafu na matusi niliyowahi kukutukana kwenye kipande cha video kilichosambaa sana kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo facebook,instagram,youtube n.k. So ningependa kuchukua nafasi hii adhimu kuweza kukuomba msamaha kwa lile jambo lilitokea kwani kusema ukweli kabisa sikuwa kwenye hali yangu ya kawaida kwani nilikuwa nimelewa sana pombe”, aliandika Dudu baya.

Baada ya hapo Planet Bongo ya East Africa Radio ilimtafuta Dudu Baya na kusema kuwa ameamua kufanya hivyo kwa sababu anampenda sana Mungu, hivyo akimkosea mtu lazima atamuomba msamaha na kwa kuwa alimsikia akilalamika kuwa ameumia (Sheta) kutukaniwa wazazi wake.

“ Mi nampenda sana Mwenyezi Mungu na kama unampenda Mungu huwezi ukapenda sana maugomvi na mtu, na ndio maana mi naweza nikamkosea mtu alafu nikamuomba msamaha, na mi mtu akinikosea natakiwa kumsamehe hata kama hajaniomba msamaha, yani mi nimeapology kwa sababu nilimsikia kwenye radio moja akisema mi nimeumia tu kutukaniwa wazazi wangu, na nilitukana hayo matusi, kwa hiyo nimeapology kwa yale matusi”, alisema Dudu Baya.

Eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364