-->

Hii ya Ray Kigosi kwangu ni mpya -Baraka Da Prince

Msanii Baraka da Prince amejibu kauli ya Ray aliyoitoa hapo jana na kutoa siri ya yeye kubadilika rangi yake, na kusema kuwa anakunywa maji mengi na kufanya mazoezi sana.

new-bk-444

Akiongea na East Africa Television/ Radio, Baraka amesema kuwa kitu hicho ni mara ya kwanza kusikia maishani mwake, kwani hajawahi kusikia popote duniani.

Ameanza kwa kucheka…..”hahahahahaaa, mi ndo mara yangu ya kwanza kusikia hiyo, sijawahi kusikia popote duniani, ila labda ni kweli (huu anacheka) ila mi sijui kama maji yanabadilisha rangi”, alisema Baraka da Prince ambaye ni mweusi.

Baraka aliendelea kusema kwamba yeye haamini kabisa katika hilo na napenda rangi yake na hafikirii kubadilisha muonekano wake, kwani hivyo alivyo mashabiki wanampenda, licha ya Ray kusema pia anafanya hivyo ili awe na muonekano mzuri kwa jamii.

“Siamini hayo mambo, na napenda rangi yangu jinsi ilivyo, sasa kwa nini nibadlishe, siamini kama watu wanapenda rangi nyeupe, mi sina rangi lakini napendwa, naperform mpaka watu wanalia, mpaka napewa tuzo, kazi nzuri ndio inafanya mashabiki wapende kazi yako na wakukubali, mbona mi bonge la HB (akimaanisha handsome boy) na weusi wangu na watu weupe nawakalisha, mi handsome”, alisema Baraka da Prince.

Akijibu post ya Godzila akimtaka Baraka da Prince akatumbukie baharini ili awe mweupe, amesema yeye na Godzila wanataniana, hivyo hana tatizo na hilo kwani pia anamchukulia kama kaka yake, hivyo haijamsumbua.

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364