Mwakifwamba : Sitowaangusha Wazee Wangu, Agombea Tena Urais
MGOMBEA wa nafasi ya Urais wa shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifwamba amefunguka kwa kusema kuwa hatawaangusha wazee waliomwamini na kumuomba agombee tena uongozi TAFF baada ya kuwa na imani naye hivyo hata waangusha bali atafanya kazi kwa nguvu.
“Ikumbukwe nilipanga mwaka huu kupumzika na kuangalia mambo ya kifamilia zaidi lakini wazee wangu ambo wapo katika tasnia hata kabla yangu wametumia sana nafasi ya kuniomba niwatumikie nami sitowaangusha,”anasema Mwakifwamba.
Mwakifwamba anagombea nafasi hiyo kwa mara nyingine baada kuwa Rais wa TAFF kwa msimu uliopita na amefanya mengi makubwa katika tasnia ya filamu kama suala la sera ya Filamu ambayo ipo wizarani ikifanyiwa mchakato.
Pia kuwaunganisha wasanii wa Mikoani kwa kuwaweka pamoja na kuweza kutambulika kwani siku za nyuma ilikuwa lazima uwe Dar ndio uigize sasa hata wasanii wa Mwanza wanaweza kuigiza na kazi zao kuuzwa sokoni bila hata kuwa na wasanii wengine waliozoeleka.
Katika kinyang’anyiroi hicho Mwakifwamba hayupo pekee yake kuna wagombea anaoshindana nao na kufanya mchuano huo uwe hai zaidi baadi mwigizaji mkongwe na mwenye nguvu katika tasnia ya filamu Issa Kipemba ‘Kipemba’ kutia maguu na wa tatu ni Babu akitokea Morogoro.