-->

Hivi Ndivyo Irene Uwoya Alivyojifungua Kwa Upasuaji Bila Ganzi

Msanii wa filamu Irene Uwoya amesema hakupenda kabisa kujifungua kwa upasuaji lakini ilimbidi afanye hivyo ili kuokoa maisha yake pamoja naya mwanaye.

IRENE UWOYA89

 

Muigizaji huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwae Krish, amekiambia kipindi cha Uhondo cha EFM kuwa wakati anaelekea hospitali kucheki afya yake na maendeleo ya mimba yake, hakujua kama ndio siku ambayo angejifungua kwa kuwa hakuwa na dalili yoyote.

“Kwanza nilikuwa sipo Tanzania, nilikuwa na siku moja toka nirudi, so kesho yake nikaenda hospitali kuangalia mimba inaendeleaje. Kiukweli namshukuru Mungu sikuwahi kusikia maumivu ya uchungu, nikaenda pale Regency, kwa hiyo dokta kuniangalia tu akasema mtoto anachungulia wewe unatembeaje?, nikamwambia mimi sijui na hapo nimevaa kiatu kirefu kweli, akaniambia toa viatu mtoto anachungulia,” alisimulia Irene.

“Wakanifanyia vipimo, lakini baadaye wakaniambia huwezi kujifungua kawaida, njia ndogo kwa hiyo inabidi tukufanyie upasuaji. Kiukweli nilitamani kujifungua kawaida. Lakini nikikumbuka ile siku nakumbuka kile chumba kilivyotisha, kitu ambacho nakumbuka sana ni ganzi, walikuwa kila wakipiga inakataa, ikabidi nifanyiwe upasuaji hivyo hivyo, yaani nilipata maumivu makali mpaka nikawa naweweseka nahisi niko Paris kwa sababu kila walichokuwa wanakifanya nilikuwa nakisikia,” aliongeza Irene.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364