Mbowe Akamatwa na Polisi, Afikishwa Kituo cha Polisi
MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe, leo Februari 20, 2017 amekamatwa na Jeshi la Polisi, Dar es Salaam wakati akienda kujisalimisha kwa ajili ya mahojiano kufuatia Mkuu wa Mkoa wa Dar, Pal Makonda kumtaja kwenye sakata la madawa.
Kamanda wa Polisi Kanda maalumu Dar es Salaam Simon Sirro amethibitisha kukamatwa kwa Mwenyekiti Freeman Mbowe.
Mwenyekiti wa Chadema Dar, Kileo amethibisha kukamatwa kwa Mbowe huku Msemaji wa CHADEMA, Boniface Makene, akisema Freeman Mbowe amekamatwa wakati akiwa njiani kuelekea kituo cha polisi kwa mahojiano. Naye Katibu wa
Kwa mujibu wa mwandishi wetu aliyepo eneo la tukio, Mbowe amefikishwa katika Kituo Kikuu cha Polisi kwa ajili ya mahojiano.
VIDEO ya Gari lililomundoa kituo cha Polisi Freeman Mbowe leo jioni