IGP Mangu Awasimamisha Kazi Askari Polisi 12 Wanaodaiwa Kujihusisha na Mihadarati
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu amewasimamisha kazi askari 12 waliotuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya wakati uchunguzi ukiendelea.
IGP huyo amewaambia wanahabari, Jumamosi hii katika makao makuu ya Polisi huku akisema kuwa Polisi ndiyo chombo kinachoongoza mapambano juu ya madawa hayo, huku akisema kuwa hatua zitachukuliwa dhidi ya askari atakayetuhumiwa.
“Tumeamua kuwasimamisha kazi wote walioguswa moja kwa moja na sakata hili, pia Polisi itachukua hatua madhubuti ikiwemo kuwapeleka mahakamani wasanii waliotuhumiwa,” alisema.
Askari hao ni wale waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda siku mbili zilizopita wakati akiwaambia wanahabari juu ya watu wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara na matumizi ya madawa hayo.
Majina ya waliosimamishwa haya hapa
1. PF 14473 SACP. CHRISTOPHER FUIME
2.PF 17041 INSP. JACOB HASHIM SWAI
3.E 8431 D/SGT MOHAMEDI JUMA HAIMA
4.E 3499 D/SGT STEVEN APELESI NDASHA
5.E. 5204 D/SGT STEVEN JOHN SHAGA
6. E.5860 D/CPL DOTTO STEVEN MWANDAMBO
7. E.1090 D/CPL TAUSEN LAMECK MWAMBALANGANI
8. E.9652 D/CPL BENATUS SIMON LUHAZA
9. D.8278 D/CPL JAMES SALALA
10. E.9503 D/CPL NOEL MASHEULA MWALUKUTA
11.WP 5103 D/C GLORIA MALLYA MASSAWE
12. F 5885 D/C FADHILI NDAHANI MAZENGO