-->

Iren Uwoya, Dogo Janja Wamfariji Johari Kwenye Msiba wa Mama Yake

Iren Uwoya, Dogo Janja Wamfariji Johari Kwenye Msiba wa Mama Yake
SO SAD! Kufuatia kifo cha mama mzazi wa Staa wa Bongo Movies, Blandina William Wilbert Chagula ‘Johari’, Bi. Asha Chagula, maeneo ya Mburahati, jijini Dar wasanii wenzake Dogo Janja na mkewe Irene Uwoya jana walipata fursa ya kumtia moyo na kumpa nguvu ambapo walimtaka asikate tamaa na achukulie ni hali ya kawaida inayoweza kumtokea binadamu yeyote, wakati wowote.

Baada ya mazishi hayo jana Alhamisi katika Makaburi ya Kisutu, Dogo Janja alisema;

“Taarifa tulizipata mapema alfajiri mimi na mke wangu, na tangu msiba utokee tumekuwa karibu nafamilia tukifarijiana. Anachokihitaji Johari kwa sasa ni faraja, tutaendelea kumfariji hadi pale atakaporudi kwenye hali yake ya kawaida.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364