-->

Irene Uwoya: Natamani Kuwa Mchungaji wa Kanisa

Muigizaji wa filamu Bongo, Irene Uwoya, amesema ndoto yake kubwa tangu akiwa mtoto ni kuwa mchungaji wa kanisa.

Irene Uwoya

Akiongea kwenye Kikaango Live cha EATV, Uwoya amedai kuwa tangu akiwa mdogo alikuwa akiomba aje kuwa mchungaji kitu ambacho hata mama yake anajua. Anadai kuwa alikuwa na uwezo hata wa kumuombea mtu na mambo yake yakanyooka.

Na sasa anadai kuwa bado anaendelea kupata ndoto za wito huo wa kuwa starling wa madhabahuni. “Natamani siku moja niwe pastor,” anasema.

“Natamani kufanya hivi lakini Mungu anisaidie nisiwe peke yangu, sitaki kucheza na Mungu. Sitaki kusema nimekuwa pastor nahubiri halafu kuna vitu bado navifanya, hiyo sitaki,” amesisitiza.

Uwoya ambaye anasali kwenye kanisa la Roman Catholic, amedai kuwa husali pia kwenye kanisa la kilokole la Pastor Chris ambalo anadai humpa mafunzo mengi.

Uwoya sio staa wa kwanza kuonesha ndoto za kuingia kwenye masuala ya uendeshaji makanisa. Hivi karibuni Nay wa Mitego naye alidai ana mpango wa kujenga kanisa lake mwenyewe.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364