Jahazi Limevunjwa na Mungu – Khadija Yusuph
Msanii wa taarabu nchini Khadija Yusuph amesema hakuna tena kundi la Jahazi Morden Taarabu kwa sasa na tayari wamegawana vitu vilivyokuwa ndani ya kundi hilo na yeye kwa sasa yupo kwa Thabit Abdul.
Akiongea ndani ya eNews Khadija amesema Jahazi limevunjwa na Mwenyezi Mungu kwa kuwa Mzee Yusuph wakati anaacha muziki alisema hata vunja kundi hilo lakini Mungu mwenyewe ndo atalivyunja na tayari dua yake imepokelewa na Mungu.
Pia Khadija amesema kwa sasa furaha ya kaka yake Mzee Yusuph imekamilika kwa sasa na dua zake pia zitakuwa zimepokelewa na Mungu kama alivyokuwa akiomba kwamba ifikie kipindi hata nyimbo zake zisiwe zinapigwa.
Bongo5