Mv Bukoba Imeua Furaha Yangu – Kala Jeremiah
Msanii Kala Jeremiah amesema inapofika siku yake ya kuzaliwa huwa ni siku ya huzuni kwake, tofauti na wengine wanaosherehekea siku zao za kuzaliwa.
Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Kala Jeremiah amesema siku hiyo ndio siku ambayo ilitokea ajali ya Mv Bukoba na kuuwa watu zaidi ya 800, hivyo huitumia siku hiyo kufanya ibada kuwaombea wahanga hao.
“Nimekuwa nikiadhimisha siku yangu tofauti sana, nimekuwa nikiadhimisha siku yangu ya kuzaliwa kama siku ya kuwaombea ndugu zetu waliopatwa na janga la Mv Bukoba, nimekuwa nikifanya hivyo kwa miaka mingi sana, furaha ya siku yangu ya kuzaliwa inamezwa na janga hilo ambalo kwanza ni janga la kitaifa pia”, alisema Kala Jeremiah.
Kala Jeremiah amesema katika kuwakumbuka wahanga hao alishawahi kwenda kutembelea makaburi ya wahanga hao na kulifanyia usafi eneo hilo, ambalo walilikuta limechakaa kwa uchafu akiwa na wasanii wenzake wa mkoa wa Mwanza.
Eatv.tv