-->

Johari Aanika wa Kumpa Penzi Lake

Mwigizaji wa kitambo kunako Bongo Movies, Blandina Chagula ‘Johari’ ameweka wazi kuwa, ni bora ajihusishe na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume ‘kapuku’ (asiye tajiri wala maarufu) kuliko kutoa penzi lake kwa staa yeyote wa Kibongo kwa sababu wengi wao ni ‘michosho’.

JOHARI65

Blandina Chagula ‘Johari’

Johari (pichani) aliliambia Amani hivi karibuni kwamba, kwa upande wake, hivi sasa kutoka na msanii au mtu maarufu ni kujidhalilisha na kujivua nguo kwa sababu anajua tabia za mastaa wengi wa Kibongo kuwa hawana mapenzi ya kweli na zaidi sana ni pasua kichwa.

“Nimejifunza mengi kuhusu kujihusisha na mapenzi na mastaa. Sasa hivi siwezi na ni bora nimpe penzi langu hata kapuku, najua wazi atalithamini na si staa maana ataniaibisha bure,” alisema Johari na kuongeza:

“Katika maisha yangu nimejifunza mambo mengi sana ikiwemo kuumizwa hivyo kwa sasa nahitaji pumziko la moyo na siyo karaha ya wanaume wasiokuwa waaminifu kama walivyo wanaume wengi mastaa.

“Unajua mastaa wengi wanaume  wanajijua ni watu wenye uwezo wa kuwa na yeyote hivyo hutumia nafasi huyo kuliza wapenzi wao jambo ambalo kwa mimi nasema nilishalitambua na sihitaji kulia jamanis. ”

Johari aliwahi kudaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji ambaye ni mkurugenzi mwenzake kwenye kampuni yao ya RJ Production, Vincent Kigosi ‘Ray’ lakini katika mazungumzo yake hakufunguka kama anamzungumzia jamaa huyo ambaye kwa sasa moyo wake umetua kwa ‘ndege mnana’ mwingine wa Bongo Movies, Chuchu Hans.

Lakini mbali na Johari, mastaa wengi wa kike wamekuwa wakilalamikia kulizwa katika uhusiano na mastaa wa kiume kuliko wao wanaume kulizwa na wanawake mastaa.

Aidha, ndoa nyingi za mastaa kwa mastaa zimekuwa hazifiki mbali na kuvunjika kuliko ndoa za mastaa na wenza wao wakiwa ni watu wa kawaida.

Mpaka sasa, staa mwingine ambaye analia ndoa yake kuvunjika kwa kuolewa na staa ni Salome Urassa ‘Thea’  ambaye ndoa yake na staa nwenzake, Michael Sangu ‘Mike’ imevunjika huku mwanaume huyo akitangaza kuoa tena hivi karibuni.

Uhusiano mwingine ambao haukudumu ni wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Wema Sepetu achilia mbali Jokate na Alikiba.

Chanzo:GPL

NUNUA FILAMU KUTOKA STEPS ENTERTAINMENT: TUNAKUFIKISHIA POPOTE PALE ULIPO:

Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.

KAMA WEWE NI MFANYA BIASHARA UNATAKA KUWA WAKALA WA KUSAMBAZA FILAMU POPOTE PALE:

Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.

Filamu Zilizotoka Hivi Sasa >>>>HIZI HAPA

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364