-->

Juma Nature Niache Kwanza -KR Muller

Msanii Mkongwe wa Bongo Fleva ambaye kwa sasa anajitambulisha kama Rais wa Rader Enteternment rapper KR Muller amemuambia msanii mwenzake mkongwe Juma Nature amuache kwanza afanye mambo yake.

KR_Mullah

KR ameyasema hayo alipokuwa akiongea na eNews ya EATV kuhusiana na ushauri aliopewa na rafiki yake ambaye waliimba wote katika kundi la TMK Wanaume family Juma Nature kwamba aangalie alijekulishwa ‘unga’ huko Rader Enteternment ambayo inamilikiwa na msanii TID.

Maneno hayo yameonekana dhahiri kumkera KR ambapo hajui kwa nini anaibuka na maneno kama hayo japo kupata ushauri si jambo baya.

”Mimi aniache tuu niendelee na mambo yangu kwani namuheshimu sana na sjui kwa nini amesema mambo yote hayo” Amesema KR.

Awali Sir Nature alisema kwamba KR asidanganyike kuitwa Rais huko aliko na akaingia kwenye mtego wa kula unga badala yake atambue kwamba ana familia na ni mtu mzima sasa hivi.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364