Juma Nature Yupo Tayari Kumkabili Diamond Platinum
Mwanamuziki mkongwe kwenye game la Bongo Fleva, Juma Nature, amesema yupo tayari kupambana na Diamond Platnumz kwenye game la muziki ‘live bila chenga’ kwenye uwanja wa mpira ili ajulikane nani anaweza zaidi.
Ameyazungumza hayo alipokuwa kwenye show ya ‘Friday Night Live’ usiku wa kuamkia leo ambapo amefunguka kwa kusema kuwa Diamond ndiye anakalia game ya muziki nchini kwa sasa, na muziki ni furaha basi anataka kupambana naye kwenye uwanja wa Taifa na mashabiki wakitazama huku kusema nani ni mshindi.
Juma Nature anaamini kuwa Diamond ndiye kaiteka game kuliko Alikiba, Nakusema ndiye anaweza kushindana naye kwenye game la muziki. Hivyo kama viongozi wapo tayari kuunga mkono na kutengeneza muziki mzuri basi waandae tamasha hilo.
Pia Nature amezungumzia kuhusu kufanya kazi na Said Fela ambapo majuma kadhaa yaliyo pita Fela alizungumzia kuhusu kufanya kazi na Juma Nature nakusema kama ikitokea ataweza kufanya naye kazi.
”Mimi sina tatizo lakini maslahi kwanza, kama kufanya naye kazi itabidi tuandikishane mkataba kwanza”Amesema Juma Nature.
eatv.tv