Ray C Hatumii Madawa ya Kulevya- Rash Don
Muandaaji wa muziki (Producer) Rash Don amesema msanii wa siku nyingi Rehema Chalamila RC anakuja na ngoma kali ambayo yeye ndo anaitengeneza kwa sasa.
Don ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na EATV katika kipindi cha E News ambapo amesema kwamba msanii huyo ana nafasi kubwa ya kufanya vizuri kutokana na mabadiliko chanya ambayo yanaonekana kwa hivi sasa.
”Nilikuwa ‘inspired’ sana kutengeneza ngoma na Ray C kwa hiyo tulipokubaliana kufanya hivyo nimeamua kujitolea kutengeneza wimbo huo”-Amesema Don
Kuhusu suala la Ray C kurudia kutumia madawa ya kulevya Don amesema hajawahi kumwona akifanya hivyo na kwa hali aliyonayo kwa sasa hatumii tena madawa hayo kama anavyozushiwa na baadhi ya watu.