Kajala Adaiwa Kunasa Ujauzito wa Kigogo
DAR ES SALAAM: Good news? Huenda mambo yanaweza yakawa yamejipa kwa mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’ kwani kuna taarifa zinadai kuwa mwigizaji huyo amenasa mimba ya kigogo serikalini.
Chanzo makini kilicho karibu na staa huyo ambaye ana mtoto mmoja aliyezaa na prodyuza mkongwe Bongo, Paul Matthysse ‘P Funk’ (Paula), kimepenyeza ubuyu huo kuwa Kajala ana mimba ya zaidi ya miezi mitano na amegusiwa kuwa ni ya kigogo serikalini ambaye hataki kumtaja jina.
“Hivi hamna habari? Kajala mbona mjamzito. Tena yeye alianza kunasa kabla hata ya Wema, nashangaa mnakomalia kuripoti mimba ya Wema tu, Kay mmemuacha na kigogo wake,” kilimwaga ubuyu chanzo hicho.
Baada ya kupewa ubuyu huo, juzi Alhamisi, mwanahabari wetu wakati anaanza kuichimba habari hiyo, alitembelea kwenye ukurasa wa Instangram wa Kajala na kukutana na ujumbe ulionesha dhahiri kuwa mwigizaji huyo anajiandaa kuitwa mama kwa mara nyingine.
“Hey IG…do me a favor…help me to choose a name of my new baby coz Pau wants a name with P in the beginning and mimi sitaki..” aliandika Kajala akiwataka wafuasi wake katika mtandao huo wamsaidie kuchagua jina la mtoto wake ajaye kwani Pau (Paula) anataka jina linaloanza na herufi P lakini yeye hataki.
Alipopigiwa simu na mwanahabari wetu kuhusiana na ujumbe huo sanjari na taarifa za kuwa ni mjamzito wakati gazeti hili linakwenda mitamboni, Kajala alikata simu. (Huenda alikuwa sehemu ambayo hakuweza kuzungumza, bila shaka ataona habari hii na kutoa ufafanuzi zaidi kwani ni jambo la heri.)
Chanzo: GPL