-->

Wema Sepetu Awafunda Wabunifu Chipukizi

WEMA SEPETU32

MISS Tanzania 2006, ambaye pia ni mwigizaji wa filamu za bongo, Wema Sepetu, amewataka wabunifu chipukizi wa mavazi na mitindo nchini walitumie vizuri jukwaa la mitindo la Lady In Red Fashion Show 2016, ili wafikie malengo waliyojiwekea.

Wema alitoa rai hiyo alipokuwa akizungumza nao kuhusiana na onyesho litakalofanyika Januari 31, katika ukumbi wa Danken House, uliopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam.

“Kwa sasa mnatakiwa muwe wabunifu zaidi mje na vitu vya kipekee ili kazi hizo ziwe chachu na kivutio kwa wateja wenu, pia iwaongezee mashabiki wa mavazi na ajira yenu, iwe ya uhakika na soko,’’ alieleza Wema.

Naye Mkurugenzi wa Fabak Fashions na muandaaji wa jukwaa hilo, Asia Idarous, alisema jukwaa hilo ni shule na daraja la wabunifu wa mavazi na mitindo, hivyo litaendelea kuenziwa ili lizidi kuzalisha wabunifu wengi zaidi.

Mtanzania

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364