-->

Kambi Kupaa Kimataifa

MKONGWE kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Hashim Kambi amesema anamshukuru Mungu kwa kumaliza na kuuona Mwaka Mpya akiwa nchini Mare­kani huku akiahidi kuzidi kutusua kimataifa mwaka huu.

Mzee Kambi

Mzee Kambi

Akizungumza na Swaggaz kwa njia ya simu kutokea Wash­ington DC, Marekani, Kambi amesema yupo katika hatua za mwisho kukamilisha sinema mpya anayorekodi nchini humo akiwa na mwigizaji mwenzake, Charles Magali.

“Tunaendelea na kurekodi huku Marekani, kazi ni nzuri sana na naamini itazidi kunitangaza kimataifa. nimejiwekea nadhiri kwamba lazima nitafute zaidi masoko ya kimataifa kwa sasa maana hapo nyumbani nimesha­tengeneza heshima vya kuto­sha,” alisema.

Mahojiano zaidi na msa­nii huyo kuhusiana na safari ya Marekani na namna tasnia ya ui­gizaji ilivyo nchini humo, usikose kusoma jarida hili wiki ijayo.

Mtanzania

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364