-->

Lulu, Uwoya, Wema… Pisheni Njia

SINEMA mpya ya kimataifa ya Homecoming imekuja na vipaji vipya katika sinema za Kibongo, huku Magdalena Munisi akiibuka na kuwatishia amani madiva wa Bongo Muvi wanaotesa katika tasnia hiyo.

Magdalena Roy-Munisi

Magdalena Roy Munisi

Mastaa wanaoonekana kufanya vizuri zaidi Bongo Muvi kwa sasa ni pamoja na Elizabeth Michael ‘Lulu’, Irene Uwoya, Wema Sepetu, Rose Ndauka, Shamsa Ford na Aunt Ezekiel.

Magdalena ambaye katika sinema hiyo amecheza kama mpenzi wa Daniel Kijo aliyecheza kama ofisa wa benki aliyetokea Marekani na kuja kufanya kazi nchini baada ya masomo yake, lakini akajikuta akiingia kwenye mtego wa rushwa.

Viwango alivyoonyesha Magdalena katika kuvaa uhusika, uhalisia na kukopi na wasanii wenzake ni dalili za mwanzo mzuri wa mafanikio katika tasnia ya filamu za Kitanzania.

Mbali na Magdalena, wasanii wengine wapya walioonyesha maka- li yao katika filamu hiyo ni pamoja na Daniel Kijo (Abel Mshindi), aliyejipatia umaarufu katika Kipindi cha Daladala kinachorushwa na Star Tv cha jijini Mwanza.

Kijo ndiye staa wa sinema hiyo ambayo uzinduzi wake ulifanyika Desemba 29, 2015 katika Ukumbi wa Sinema wa
Century, Mlimani City jijini Dar es Salam huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Mosses Nnauye.

Wasanii wengine walioonyesha makali yao kwenye filamu hiyo ni Issa Mbura, Godliver Gordian, Michael Kauffmann
na Abby Plaatjes aliyewahi kuwa mshiriki wa Big Brother Africa (BBA) na mtangazaji wa Radio Choice FM.

Mastaa walioongeza nguvu katika filamu hiyo iliyotayarishwa na Kampuni ya Alkemist Media ni Suzan Lewis ‘Natasaha’, Hashim Kambi na Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’.

Mtanzania

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364