Kampuni 3 Zamtaka Mtoto wa Wema
Kampuni tatu zimejitokeza kutaka kumtumia kibiashara mtoto atakayezaliwa baada ya staa wa filamu Wema Sepetu kujifungua baadaye mwaka huu.
Chanzo cha uhakika kilicho karibu na staa huyo, kimesema kampuni hizo ambazo hakuzitaja kwa kushindwa kukariri majina yake, zimeshafanya mazungumzo ya awali na Wema, kwani wanaamini mtoto huyo atakuwa kivutio kikubwa.
“Hivi ninavyokuambia licha ya kampuni hizo, tayari wengine wamejitokeza na kudai watamvalisha kwa muda wa mwaka mzima mtoto huyo,” kilisema chanzo hicho.
Gazeti hili lilimtafuta muigizaji huyo na kuulizia juu ya ishu hiyo, ambapo alicheka na kudai hayuko katika nafasi nzuri kwa muda huo ili kuzungumzia suala hilo hadi hapo baadaye.
“Kwa sasa ni mapema mno kuzungumzia hilo jambo, nitaweka wazi baadaye,” alisema Wema
Chanzo: GPL