-->

Kijiweni Production Kuonyesha Filamu ya ‘T-Junction’ Agosti 11

Kijiweni Production Kuonyesha Filamu Agosti 11 mwaka huu, filamu iitwayo ‘T-Junction’ itaonyeshwa kwenye jumba la sinema lililoko Mlimani City jijini Dar. Habari hiyo imesemwa na kuthibitishwa na kampuni   ya Kijiweni Production.

Habari kamili kuhusu Kijiweni Production Kuonyesha Filamu

Akizungumza na wanahabari jijini Dar leo, Mwongozaji Mkuu wa Filamu hiyo, Amil Shivji, amesema kuwa filamu hiyo baada ya kuonyeshwa siku hiyo itaendelea kuchezwa hapa nchini na duniani kote kwani imechaguliwa pia kuwa mojawapo ya filamu za juu za Afrika ambazo zitaonyeshwa katika matamasha ya filamu nyingi Ulaya.

“Kuhusu T-Junction, ni filamu inayowahusu mabinti na jamii zao, jamii moja ikiishi kiholela. Faraja yao ni kujua wana umoja na furaha. Jamii yao inazingatia mifumo, kanuni na taratibu za utu,” alisema Shivji.

Tukio la Kijiweni Production Kuonyesha Filamu litafanyika  jijini Dar es Salamam baada ya kuonyeshwa kwenye Tamasha la ZIF lililofanyika Stonetown, Zanzibar, hivi karibuni.

Na: Denis Mtima| GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364