-->

Kingwendu: Ningepewa Hiki Ningekuwa Level Moja na Diamond na Alikiba

Mchekeshaji maarufu nchini, Kingwendu amesema kama nyimbo zake zingepata promotion ya kutosha, angekuwa anashindana na wasanii wanaofanya vizuri kwa sasa, Diamond na Ali Kiba.

Kingwendu.._full

Kingwendu ambaye alikuwa katika show za mwisho wa mwaka nchini Ujerumani hivi karibuni, ameiambia Bongo5 kuwa hali hiyo inamfanya aanze kutafuta maneja ili aweze kusimamia kazi za muziki wake.

“Mwaka jana nimetoa nyimbo tatu lakini zote hazikupata airtime ndio maana hazikufanya vizuri lakini kwa sababu ni nyimbo nzuri zingepata airtime ningeshindana na akina Ali Kiba na Diamond ambao wanafanya vizuri,” amesema.

Aliongeza, “Sijakata kataa, mwaka huu kuna kazi mpya nimeziandaa pamoja na video mpya. Pia nikifanikiwa kupata meneja wa kusimamia muziki wangu natumaini nitafika mbali sana kwa sababu muziki wa sasa ni mipango tofauti na ule wakati nimetoa Mapepe.”

Kingwendu anadai anapenda kufanya muziki na filamu kwa pamoja kwa sababu vyote vinamlipa vizuri.

Chanzo: Bongo5

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364