-->

Wastara: Nahisi Mauti Yapo Karibu Yangu

WASTARA34

Soma vizuri ili uelewe vizuri
Naanza kwa kumshukuru mungu wangu anaenipa pumzi ya bule mpka mda huu
Sina budi kusema hya nitakayoyasema kwa ajili mwaka mpya unaonza kesho
Ni miaka 4 na miezi 6 leo imetimia toka furaha yangu ilipoingia dosari
Mungu alinipa mtu wa kunipa furaha couz kilakitu Alhamdulilah nilikuwanacho kulingana na nafasi yangu lakini sikuwa na furaha lakini furaha hiyo aikudumu nakumbuka ilikuwa mwezi 6/ 2011 marehemu sajuki alipoanza kuumwa ndipo furaha ilipoanza kupotea couz sikupta nafuu wala moyo wangu kupumzika mpka leo tal 31 nimejaribu kutafuta furaha kila sehemu kila njia ila imeshindikana, na mungu nae anaendelea kunipa mitihani ya maradhi ambayo naamini yatapona na kuisha soon ila kuishi katika mazingira hayo kwa mtu mwengine angekuwa kama kizee hata kuchana nywele ingekuwa shida ila katika maisha ya maumivu na Sajuki siku moja aliniambia mke wangu mi naumwa ila sipendi kukuona ukiwa mchafu na pia usinizuie kwenda kokote sababu nitakufa siku yoyte tutumie mda uliobakia kufanya kile kitu moyo unataka .
Nami kwasasa naishi hivyo nahisi mauti yapo karibu yangu sana hivyo kile moyo wangu unataka ndicho nakifanya hata moyo ukiniambia inuka na maumivu yako nipeleke baharin basi naupeleka uko ukisema nipeleke disco naupeleka uko ukisema nikakeshe msikitini naupeleka uko hivyo sitabariki na sipendi kuishi ili mtu anione nina maumivu nalazimisha furaha japo haipo hivyo mnisamehe wale wote msionielewa kokote mkinikuta mniche tu sifanyi kitu kumkera mtu i need rea lif ya moyo wangu maskini unanivuja damu kila siku natamani nifanye lolte ili upumue hakuna kitu kibaya kama kupoteza furaha na tumain unaishi kma uko dunia ya peke yako nimeongea hya ili muelewe hisia zangu kuwa hta ukiongea kitu ambacho sijakifanya sihusiki au kunitafsiri vibaya naumia mara 2 nahisi kma na wew ni mmoja ya wale wasiopoenda kuona nikifurahia uwepo wangu duniani
Viongozi wangu ndugu jamaa wasanii wenzengu na mshabiki wangu nawaomba kwa pamoja mpige goti kuniombea 2016 moyo wangu upate furaha ya kudumu upate dawa ya maumivu upate tabasamu la kweli na sio feki ninalotoa sasa aniondoshee maradhi yote
moyo wangu unahitaji realif maskin mwaka 2016 uwe na neema kwetu sote ameen

Wastara aliandika juzi kwenye ukurasa wake mtandaoni.

Amen

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364