Kituo Cha kusaidia Watu walioathirika na Dawa za Kulevya cha Life and Hope Sober House kilichopo Bagamoyo kimekanusha kuwepo kwa taarifa juu ya msanii wa miondoko ya Hip Hop, Rashid Makwiro maarufu kama Child Benz kutoroka kituoni hapo.
Akikanusha tuhuma hizo za kutoroka kwa Msanii huyo, Mkuu wa Kituo hicho, Al-Kareem Bhanji ameeleza kuwa Chid Benzi aliondoka kituoni hapo baada ya kufuata taratibu zote za uongozi pale alipoonekana yuko sawa.
“Ukweli ni kwamba Chid hakutoroka kituoni hapo bali alifuata taratibu na baraka zote za uongozi zilizotolewa baada ya kuonekana yuko sawa”amesema Bhanji
Pia amekanusha kuwepo kwa taarifa ya kuwa Babu Tale alimtelekeza Chid kituoni hapo.
“Babu Tale alitoa ushirikiano wa hali ya juu katika kusaidiana kama mnavyojua ukweli mpaka kumleta Chid kituoni. Tulikuwa muda wote tunashirikiana naye” ameendelea kueleza Bhanji
Chid Benzi alikaa kituoni hapo kwa takriban Mwezi Mmoja na Nusu na kuruhusiwa na uongozi wa kituo hicho baada ya hali yake kuona inaridhisha.