-->

Koffi Olomide Akamatwa Nyumbani Kinshasa

Mwanamuziki maarufu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC amekamatwa akiwa nyumbani kwake mjini Kinshasa.

Mwanamuziki wa Kongo Koffi Olomide

Mwanamuziki wa Kongo Koffi Olomide

Wiki iliyopita Olomide alitimuliwa kutoka nchini Kenya baada ya video kuonyesha akimpiga teke mnenguaji wake wa kike katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta baada yake kuwasili nchini humo.

Lengo la ziara ya Kenya alipangiwa kutumbuiza mashabiki wake Bomas of Kenya siku ya Jumamosi lakini tamasha hiyo lilifutwa na mamlaka.

Koffi amekamatwa kwa agizo la mwendesha mashtaka huku kukiwa na matamshi ya wanaharakati wa haki za kibinadamu wakitaka afunguliwe mashtaka kufuatia kitendo chake cha kumpiga ‘stage show’ wake.

Aidha baada ya show ya Kenya kusitishwa alikamatwa na maafisa wa polisi na siku iliyofuata asubuhi akaingizwa kwenye ndege na kurejeshwa Kinshasa.

Chanzo BBC.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364