-->

Lady Jaydee na EFM Wameingia Kwenye Ubia Gani?

Wenyewe wanasema ‘Huu Mchezo Hauhitaji Hasira’.

Ni mchezo upi huo? Usemi huu ulianza baada ya EFM kuwapora watangazaji wawili wa Clouds FM, Gerald Hando na Paul James kabla ya wao nao kuporwa mtangazaji wao, Gardiner G Habash.

JIDE244

Na sasa movie linaendelea kunoga. Lady Jaydee anayefahamika kuwa mgogoro mzito na Clouds FM na aliyekuwa mke wa Gardiner, amejiunga na EFM katika mradi ambao ni wao pekee wanaujua kwa sasa.

Sitaki kuamini kama Lady Jaydee anaweza kurejea tena kwenye kazi yake ya utangazaji lakini kwa inavyoonekana, kuna kitu wamepanga kukifanya.

Jaydee alishare picha na video kadhaa zinazomuonesha akitembezwa na kutambulishwa kwenye studio za EFM.

“HuuMchezoHauhitajiHasira #NdiNdiNdi Efm feat Jide,” aliandika Jide kwenye picha moja.

Kila mtu anasubiri kujua nini hasa Lady Jaydee na EFM wamepanga kukifanya.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364