-->

Mafufu Adaiwa Kuzabwa Kibao na Mkewe

Kali tuliyoinasa inamhusu msanii maarufu wa filamu Bongo, Jimmy Mafufu ambaye inadaiwa juzikati alijikuta akinaswa kibao na mkewe baada ya kumsifia msichana aliyemuona kwenye TV.

Jimmy-mafufu2

Chanzo ambacho ni ndugu wa mke wa Jimmy kilichoomba hifadhi ya jina lake kilidai kuwa, siku hiyo walikuwa wakitazama filamu kwenye TV, Jimmy akaonekana kuvutiwa na mdada mmoja na kuanza kumsifia, jambo lililomkera mkewe aliyerusha kibao kilichotua shavuni.

“Ni mambo ya wivu maana mke wa Mafufu kwa wivu hajambo,” alisema mtoa habari huyo.
Jimmy alipotafutwa kuzungumzia madai hayo alisema: “Jamani kama ningepigwa na kimada ingekuwa ni tatizo lakini kam nimepigwa na mke wangu tatizo liko wapi?”

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364