Linah Akanusha Kutoka Kimapenzi na Billnas
Msanii wa bongo fleva Linah Sanga ambaye siku za karibuni amekiri wazi kuwa mapenzi yamemuathiri katika kazi yake ya sanaa na kufanya watu kufuatilia zaidi maisha yake ya mahusiano kuliko kazi zake amefunguka na kuweka sawa kuwa hatoki kimapenzi na msanii Billnas.
Kupitia kipindi cha eNEWS tulitaka kufahamu ukaribu uliopo kati ya Linah Sanga na Billnas ndipo hapa Linah alipoweka wazi kuwa yeye kumpa support Bill Nas katika kazi yake mpya kwa kuiweka link ya ngoma ya Chafu pozi kwenye bio yake Instgram ni kwa kuwa anampa support msanii huyo na si jambo la ajabu kwa wasanii kupeana support lakini haina maana kuwa wanatoka kimapenzi.
“Billnas aliniomba niweke link yake wimbo wake baada ya kufanya video, hivyo kwa kuwa ni msanii mwenzangu niliamua kumpromote, mimi na Bill Nas imekuwa big dili lakini ni mambo ya kawaida kabisa ndiyo maana unaweza kuona msanii kama Vanessa Mdee anaweza kuweka link ya Weusi na hata Weusi wanaweza kuweka link ya Vanessa hivyo ni mambo ya kawaida” alisema Linah Sanga.
>>>NUNUA FILAMU KUTOKA STEPS ENTERTAINMENT: TUNAKUFIKISHIA POPOTE PALE ULIPO:
Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.
KAMA UNATAKA KUWA WAKALA WA KUSAMBAZA FILAMU POPOTE PALE:
Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.
Filamu Zilizotoka Hivi Sasa >>>>HIZI HAPA