-->

Lulu Diva Alilia Uolewa

MUUZA sura kwenye video za Kibongo ambaye pia ni muigizaji, Lulu Abbasi ‘Lulu Diva’ amenyetisha kuwa kutokana na changamoto za kimaisha anazokutana nazo anatamani kuwekwa ndani muda wowote kama mke jambo ambalo anafikiria linaweza kumsaidia kwa kiasi fulani kimaisha kwa sababu atakuwa anaambulia angalau hata pesa ya meza.

DIVA111

AKipiga stori na BBM, Lulu ambaye hivi karibuni alitupiwa vitu nje na mwenye nyumba wake kisa kumshtaki polisi mtoto wake aliyedai alimwibia rice cooker na vitu vingine, aliendelea kufunguka kuwa hali hiyo imemfanya kujikuta wakati mwingine akitokwa machozi lakini zaidi anamuomba Mungu amsaidie ili mpenzi wake aliyemuahidi kumuoa ‘soon’ kwa kufunga naye ndoa ati         mize ahadi yake.

“Kwa kweli maisha kwa sasa yamebadilika na kuwa magumu sana, ninajitahidi kukomaa lakini changamoto bado ni nyingi, ninatamani kuolewa, unajua nikiwa ndani japo nitaendelea na mambo yangu lakini pale ninapokwama nitaambulia hata pesa ya pango,” alisema Lulu Diva.

Chanzo:GPL

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364