-->

Lulu: Mama Amenistiri Sana!

LULU567

STAA wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa hakuna wa kumthamini na kumheshimu hapa duniani zaidi ya mama yake kwani ndiye mtu pekee aliyempa faraja ya kweli katika maisha magumu aliyopitia.
Akizungumza kwa uchungu Lulu alisema, mama yake pekee ndiye aliyemuona ana thamani wakati watu wengine wakimuona ni mchafu wa maneno na hafai kabisa kwa vitendo.
“Daah kuna watu walinibeza kwa maneno machafu na kuniona sifai kabisa katika dunia hii lakini mama yangu alinikingia kifua na amekuwa zaidi ya faraja kubwa katika ulimwengu huu,” alisema Lulu.
Chanzo: GPL

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364