-->

Chuchu Hans Akanusha Kugombana na Johari Kisa Ray

Staa wa Bongo Movies, Chuchu Hans amekanusha kugombana na Johari Chagula baada kuibuka madai kwenye mitandao ya kijamii kuwa wawili hao hawaelewani kisa Vicent Kigosi aka Ray.

CHUCHU23

 

Chuchu aliyesema pia kuwa uhusiano wake na Ray hauna tatizo, amekiambia kipindi Take One cha Clouds TV Jumanne hii kuwa, hana tatizo na Johari na mara nyingi wakikutana husalimiana.

“Kitu ambacho nakijua mimi kama mimi, Johari ni business partner na Ray,” alisema. “Ni watu wa karibu kwa sababu wameitengeneza kampuni ya RJ mpaka hapa walipofikia sio sehemu ya kawaida na sio kazi rahisi. Johari ni msanii mwenzangu na mimi kila mtu ni rafiki yangu, nikikutana naye tunasalimiana halafu kila mtu anaendelea na mambo yake,” alisema Chuchu.

Katika hatua nyingine Chuchu alisema Ray anapenda sana watoto hivyo watoto wake wawili anawachukulia kama wanae.

Bongo5

Comments

comments

Post Tagged with , ,

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364