-->

Madee Achomoa Kuchoma Gari Lake Baada ya Kichapo

madee34

Baada ya Arsenal jana kupigwa kichapo cha bao moja mtungi na Chelsea, msanii wa bongo fleva Madee amechomoa kuchoma gari lake kama alivyoahidi na kusema yeye hana utajiri huo wa kuchoma gari na hata kama angekuwa nao asingeweza kufanya hivyo.

Madee jana alipost kwenye Account yake Instgram na kudai kuwa kama Arsenal watafungwa na Chelsea basi angechoma moja ya gari lake, lakini baada ya kuchezea kichapo Madee amekana kuchoma gari lake moja na kusema hawezi kufanya jambo hilo.

Kupitia Account ya Twitter leo Madee ameandika ujumbe huu “Sina utajiri huo. mpaka kufikia hatua ya kuchoma gari…na hata kama ningekua tajiri vipi. .nisingefanya upumbavu huo”. Alisema Madee

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364