Sitaki Kusikia Siasa Tena- Mzee Yusuf
Mzee Yusuf mwaka jana alikuwa na nia ya kugombea ubunge kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi katika jimbo la Fuweni Zanzibar lakini baadaye alipigwa chini kwenye kura za maoni na badala yake alikuwa akionekana kwenye kampeni za chama hicho akitoa burudani kama ambavyo wasanii wengine walikuwa wakifanya.
“Sahizi nasema ukweli kabisa sitaki kusikia kitu kinaitwa siasa, na wala mwaka 2020 siwezi kugombea nafasi yoyote ile ya uongozi labda itoke nichaguliwe tu ila mimi na siasa hapana, kwa sasa mimi nataka kuangalia masuala ya biashara niwe mfanyabiashara mkubwa kama wakina Dr Reginald Mengi, Azam, Mo Dewji yaani nataka kushindana na watu hawa kibiashara ila sio siasa sitaki kusikia kabisa”. Alisema Mzee Yusuf
EATV.TV