-->

Majuto: Kuhiji Kunanipa Wakati Mgumu wa Kuigiza

MSANII nguli wa vichekesho nchini, Amri Athumani ‘King Majuto’, amesema anapata shida na aina ya uigizaji kwa sasa baada ya kwenda kuhiji na kuwa Alhaji.

majuto22

Akizungumza jana katika Ofisi za New Habari, King Majuto, alisema   unapokwenda kuhiji unatakiwa kufuata sheria za dini na mambo yenye hekima na kujiepusha na vitu ambavyo havitakiwi kwenye dini.

“Vitu hivi vinakuwa ni vigumu  kuviepuka na hasa katika kazi zetu kwani unakuta unaigiza na mtu kama mke wako na sisi sheria zetu haziruhusu kuwa naye karibu hiyo ni moja ya changamoto kubwa ambayo naikwepa,” alisema Majuto.

Hata hivyo, mchekeshaji huyo alisema kuwa anatimiza ahadi zote za dini yake na kujitahidi kuepuka vitu ambavyo havitakiwi japokuwa ni vigumu.

Mtanzania

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364