Makonda Agoma Kumuomba Radhi
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amegoma kuomba msamaha kutokana na kudai kuwa hakukivamia kituo cha Clouds Media na walinzi wake kama ilivyosambaa bali watu hawakuelewa kilichotokea.
Akiongea na waandishi wa habari leo Jumatano mbele ya viongozi Jukwaa la Wahariri (TEF) na Ruge, Makonda amesema, “Ndugu waandishi wa Habari na Wahariri kile ambacho Katibu amekisema hakitatokea kwenye kinywa changu, sitaomba radhi.”
“Naelewa na watu wote wanajua mahusiano niliyokuwa nayo na Clouds hakuna asiyejua upendo nilionao na watu wa Clouds. Tuendelee kufanya kazi, mimi na Ruge ni marafiki wa muda mrefu tuliyotofautiana sisi tuyashughulikie kwa engo yetu. Tusiingize taasisi yote kuwaingiza wananchi ambao hawana hatia, hawana kosa kwa sababu ya mahusiano yangu na Ruge,” ameongeza.
Hata hivyo katika mkutano huo hakuna muafaka sahihi ambao umeweza kupatikana na umewaacha waandishi wa habari waliokuwepo njia panda.
Bongo5