Makonda Ahojiwa na Kamati ya Madaraka ya Bunge
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amefika mbele ya kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge baada ya wito wa Kamati hiyo kumtaka ajibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge.
Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Bunge imeeleza kuwa Makonda anahojiwa kutokana na matashi aliyoyatoa Februari mwaka huu jijini Dar es Salaam yanayodaiwa kulidharau bunge.
Makonda aliitwa baada ya Bunge kuazimia kumhoji kiongozi huyo, mnamo Februari 8 mwaka huu.
Mwananchi