-->

Mali za Jide Zazua Kizaazaa!

LADYJAYDEE

Jambo limezua jambo! Siku chache baada ya kukabidhiwa talaka na aliyekuwa mumewe, Gardner G. Habash ‘Captain’, mali za mrembo wa nguvu, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ zinadaiwa kuzua kizaazaa baada ya kusemekana kutokea mvutano wa baadhi ya ndugu wa mwanamuziki huyo kutaka amgawie mtalaka wake  huyo, Amani lina ubuyu kamili.

TUANZE NA TALAKA
Baada ya Jide au Lady Jaydee kuishi kwa zaidi ya miaka 9 ndani ya ndoa na Gardner, Februari 12, mwaka huu, wawili hao walivunja rasmi ndoa yao katika Mahakama ya Mwanzo Manzese- Sinza jijini Dar na kila mmoja kupewa hati yake ya talaka hivyo hadi leo zimepita siku 35 tangu walipotengana.

USTAWI WA JAMII WALIAMUA
Licha ya kupeana talaka, awali vikao vya ugawaji wa mali katika Idara ya Ustawi wa Jamii, Magomeni jijini Dar viliamua kuwa Gardner hakuwa na chake katika mali kwa kile kilichoelezwa kwamba, alikuwa kama mwajiriwa katika kazi za sanaa za Jide.

nyumbaMjengo wa Jide ulioko maeneo ya Kimala.

TWENDE KWA NDUGU WA JIDE
Ndugu wa Jide aliyejitambulisha kwa jina moja la Jack, aliliambia Amani kwamba, baadhi yao wamecharuka na kumwambia Jide atende haki kwa kumgawia mwenzake (Gardner) kwani hawana kinyongo naye na walimtambua kama mume kwa kipindi chote cha ndoa yao.
“Ni mvutano! Kuna ambao wanataka Jide agawe asilimia hamsini kwa hamsini ya mali zake kwa vile licha ya kwamba alikuwa kama meneja wake katika kazi, lakini kwa upande mwingine alikuwa ni baba wa familia. Lakini kwa upande wa ndugu wa Gardner, hatujasikia wakisema lolote.”

WENGINE HAWATAKI KUSIKIA
“Hata hivyo, kuna ambao hawataki kusikia Gardner anapewa hata senti tano kwani wanaamini ndugu yao (Jide) hana hatia hivyo Gardner ale jeuri yake maana alishindwa mwenyewe kuheshimu ndoa na kusababisha migogoro,” alisema ndugu huyo na kuongeza:

WATOLEANA MANENO MAKALI
“Hali imefika pabaya, imefika mahali wale ambao wanataka Jide asimpe chochote Gardner wanawapa maneno makali wale wanaotaka apewe. Kila mmoja anavutia kwake.”

Jaydee's carKESI YATAJWA
Kwa mujibu wa chanzo chetu kingine cha habari, baadhi ya ndugu hawaridhiki na kizaazaa hicho hivyo kutaka kumshawishi Gardner akafungue madai ya mali mahakamani ambapo wanaamini atapata haki yake.
“Wamekasirika! Wanaona bora wamtafute Gardner wamuume sikio aende mahakamani,” kilisema chanzo hicho.

JIDE BIZE NA PROJEKTI MPYA
Wakati ndugu hao wakisigana hadi kutoleana maneno makali, imeelezwa kuwa Jide ‘ameziba’ masikio akiwa ameelekeza nguvu zake katika projekti yake mpya ya Naamka Tena.
“Wamempelekea taarifa za mvutano, Jide hataki hata kuwasikiliza. Yupo bize na projekti yake ya Naamka Tena, si unajua zimebaki siku chache arudi upya kwenye soko? Hawajibu kama atamgawia mali hizo au la,” kilisema chanzo.

jide rangerJide akiwa na mkoko wake aina ya Range Rover Evoque.

JIDE HUYU HAPA
Jitihada za Amani kutaka kujua undani wa habari hiyo ziligonga mwamba kufuatia simu ya Jide ya mkononi kuita bila kupokelewa.
Hata hivyo, Amani lilitumia njia ya meneja wake aliyeomba hifadhi ya jina na kufanikiwa kumpata Jide waliyekuwa naye pamoja ambapo alikiri kutokea kwa mvutano huo wa ndugu lakini akaomba aachwe kwani yupo bize na shughuli za ujio wake mpya.
“Jamani mvutano ni wa kawaida. Mimi nipo bize na ujio wangu mpya, mbona hamniulizi kuhusu kazi yangu mpya ya Naamka Tena? Kuhusu mali mimi naheshimu uamuzi wa Ustawi wa Jamii,” alisikika Jide.

GARDNER SASA
Baada ya kumalizana na Jide, Amani lilimgeukia Gardner, mtangazaji maarufu Bongo wa Redio EFM ili kumsikia anazungumziaje kuhusu mvutano huo wa mali na namna ambavyo baadhi ya ndugu wa Jide wanamtetea.
murado la jide“Hivi kuna ndugu wana huruma hiyo? Mungu awabariki sana. Kwa upande wangu mimi namshukuru Mungu ni mzima wa afya, napambana kutafuta maisha yangu. Sina mpango wa kudai mali, najua Mungu atanipa tu,” alisema Gardner.

MALI ZENYEWE NI ZIPI?
Mali ambazo zipo mikononi mwa Jide hadi sasa ni pamoja na nyumba zilizopo Tegeta, Kimara-Temboni na Kiwalani jijini Dar. Pia kuna shamba (haikujulikana ekari ngapi) lililopo Bagamoyo, Pwani.
Gari aina ya Nissan Murano analo Jide,  Range Rover Evoque analo Jide na basi lililokuwa likitumiwa kubebea vyombo na wanamuziki kwenye Bendi ya Machozi.
Jitihada za kujua thamani ya nyumba na magari ilishindikana baada ya mwenye uelewa huo, Jide mwenyewe kutoweka wazi.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364