-->

Mama Fisso ‘The Iron Woman’ Anayepigania Tasnia ya Filamu

Mama Fisso akihutubia katika uzinduzi wa Tuzo za TAFA New Africa Hotel

Mama Fisso akihutubia katika uzinduzi wa Tuzo za TAFA New Africa Hotel

MWAKA 2015 umemalizika na kuingia mwaka 2016 kukiwa na mafanikio kibao lakini kuna mashujaa waliosaidia tasnia ya filamu kuweza kuwa katika ramani na muonekano wenye hadhi ya kimataifa na kitaifa basi FC imeangazia na kumuona mtu mwenye mchango mkubwa katika tasnia ya filamu ni Bi. Joyce Fisso ‘Mama Fissoo’
Kwetu tumemuona kama The Iron Woman’ Mwanamke wa Chuma anayepigania tasnia ya filamu ndani na kimataifa na kila ambapo amekuwa akishiriki katika mchakato wa filamu lazima aongelee maslahi ya tasnia ya filamu na kuijengea uwezo katika maendeleo ya kwenda mbele kitaaluma na kimaslahi.
Mama Fisso ni katibu mtendaji wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania ambaye toka kuingia kwake katika taasisi hiyo iliyoundwa kwa sheria ya Tanzania ya mwaka 1976 namba 4, mabadiliko makubwa sana yamefanyika na Filamu kupata hadhi yake.
USHIRIKIANO NA WADAU
Mama Fisso ‘The Iron Woman’ alipoingia tu aliwatafuta wadau wa tasnia ya filamu kwa kukagua ofisi zao sambamba na vifaa vyao akiwashauri jinsi ya utengenezaji wa filamu bora na kuweza kuzitangaza kimataifa, ni mtendaji pekee ambaye hata ukimwamsha usiku wa manane ukimuuliza kuna kampuni ngapi za utengenezaji filamu atakujibu.
Pia ukimuuliza kuna kampuni ngapi za usambazaji atakujibu bila kigugumizi kwani tayari ameweza kufanya ziara na kufika kila kwa mdau wa tasnia ya filamu na kukagua vifaa sambamba na utendaji wa kampuni husika hivyo ni mtendaji anayewajua wadau wake .
Awali nilikuwa sijui kwanini kila mtu anapenda kusema akiwa Location ‘Mama Fisso’ kumbe ni kulingana na utendaji wake makini kwa watengenezaji wa filamu ambao wamekuwa wakivunja sheria kwa kutofuata maadili ya Tanzania jambo ambalo linafanya kuwa na filamu zenye maadili.
Amekuwa balozi mzuri kwa watengenezaji wa filamu Swahilihood kwa kutoa mialiko mbalimbali inayohusu filamu ikiwa ya ndani na nje katika matamasha ya filamu na tuzo mbalimbali ikifika kwa Mama Fisso lazima wanaostahili watapewa.
Lakini tumeshuhudia pale ambapo Mama Fisso akitoa fedha zake mwenyewe kuwezesha wadau kufanikisha mambo yao ya kimaendeleo hasa katika uelimishaji katika semina na mafunzo mbalimbali kwa kuwashirikisha wadau kutoka nje na ndani ambapo tayari ujuzi unaongezeka kwa watendaji wetu.
Toka kuwepo kwa bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza wasanii hawajawahi kushiriki katika bajeti ya Wizara yao husika lakini Mama Fisso ameweza kuwapeleka Wasanii Bungeni na kushuhudia Bajeti ya Wizara yao ikiwakilisha Bajeti yao ni hatua kubwa sana.
Aidha Mama Fisso amekuwa akishiriki katika makongamano mengi sambamba na kufundisha Fani kama Uongozaji wa Filamu, uigizaji na mengineyo kitu kinachomfanya awe tofauti huduma hii amekuwa akitoa bure kimsingi iendane na ratiba za kazi zake sisi kwetu Tunamwita Mwanamke wa Chuma anayepigania tasnia ya Filamu Swahilihood.
Mama Fisso kama kiongozi mtendaji ameijenga Bodi ya filamu kuwa na watendaji wenye kasi kubwa wanaotumia muda wao kuhudumia wadau wa filamu kila wanapofika katika ofisi hizo kwa kuhudumiwa kwa wakati tena kwa ufanisi.
Sasa bodi inatoa madaraja katika filamu zetu, lakini kitu ambacho ni cha kujivunia pale ambapo wadau wameipokea Elimu kutoka katibu wetu na kuiheshimu kwa kuitii ukipita mtaani na kuona sinema isiyo na maadili lazima utasikia wadau wakisema “Hii imepita kwa Mama Fisso kweli,”
Inaonyesha wazi uelewa wa wadau na imani kwa Mama Fisso kwani unapofuata sheria wewe ni rafiki yake na ukipindisha sheria atakuelimisha tena kwa upendo bila utata ni kiongozi mlezi kwa wasanii.
Uimara wa Taff una mchango mkubwa wa Mama Fisso kwani ni mshauri pia mpiganaji mwenye mapenzi na tasnia ya filamu akiona inasonga mbele leo kila mtu hawezi kutengeneza filamu bila kufika bodi ya filamu kukaguliwa na kuendelea na shughuli zake.
Tunafurahi kuona Taff inakuwa na TAFF TRUST FUND mfuko ambao Mama Fisso anaupigania na kuhakikisha unaweza kutuna na kuwa msaada kwa Wasanii na wadau wa filamu kwani kila siku anaongelea jinsi ambavyo mfuko huo unaweza kuwa na fedha za kutosha.
Mama Fisso amekuwa akiunga mkono harakati za wadau wakubwa wanaokuza tasnia ya filamu kama vile mradi wa ukuzaji wa vipaji kama vile Tanzania movie Talent (TMT) mradi ambao umefanywa na kampuni ya kizalendo ya Proin Promotions ya Jijini Dar es Salaam.
Bila kusahau kusahau alifanikisha uwepo wa tuzo za Tafa ambazo zimefanyika mwaka huu na kufana ikiwa sambamba na uzinduzi wa kanuni za filamu mwaka 2013 na Makamu wa Rais Dr. Bilal unaona jinsi gani tunajivunia kumwita The Iron Woman Mama Fisso.
Yapo mengi yana mchango wake The Iron Woman Mama Fisso Urasimishaji wa Filamu, kuwezesha Makongomano ya filamu kufanyika kila uchwao yote ni kwa ajili yake amejenga mahusiano mema kati ya wasanii Wadau wa filamu na serikali nab ado ana mengi anayopigania katika tasnia ya Filamu.
Tunafunga mwaka tukimtangaza kama Mwanamke wa Chuma mpigania Tasnia ya Filamu Swahilihood hatuna cha kumpa zaidi ya kutambua nafasi yako na Juhudi zako Mama Fisso ‘The Iron Woman’ Wasanii na wadau wote wanajua jinsi gani mpiganaji huyu alivyoiweka tasnia juu na kutambulika.

Ripoti na Filamucentral

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364