-->

Lulu: Tekno Alijigonga Kwangu

STAA wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameendelea kukanusha ‘ubuyu’ ulionea kuwa alivunja amri ya sita hotelini na msanii wa muziki wa Nigeria, Tekno Miles, akitoa maelezo yaliyotafsiriwa kuwa, kumbe mwanamuziki huyo ndiye aliyejigonga kwa mkali huyo wa sinema za Kibongo.

LULU289

Lulu alilazimika kukanusha habari hizo kufuatia kusambaa kwa picha zake na jamaa huyo ambaye ni ‘hitimeka’ wa Ngoma ya Duro, zikiwaonesha wakiwa wamekumbatiana usiku wa Mkesha wa Mwaka Mpya 2016 ambapo Tekno aliangusha shoo ‘hevi’ kwenye Ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga jijini Dar, kabla ya kudaiwa kwenda ‘kumbonji’ wote katika Hoteli ya Serena iliyopo Posta.

Hata hivyo, kabla ya kuenea kwa picha na habari ya Lulu na Tekno, chipukizi wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ naye alihusishwa na kulala na mwanamuziki huyo hivyo kuibuka kwa utata na maneno mengi yaliyolenga kuchochea bifu kati ya warembo hao wa Kibongo.

Ili kumaliza ubishi huo, Amani lilimpa nafasi Lulu ili kueleza kile anachokifahamu katika sakata hilo ambapo alifunguka: “Kama nilivyoeleza kwenye kurasa zangu za social media (mitandao ya kijamii), nasisitiza, nilikutana na Tekno kwenye shoo yake ukumbini.

“Yeye (Tekno) ndiye alikuja kunisalimia kwenye meza yangu na siyo mimi niliyemfuata. Nilikwenda kwenye shoo yake kama shabiki wake na siyo vinginevyo na picha alipiga na watu wengi si mimi tu.”

Chanzo: GPL

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364