-->

Profesa Jay Ashinda Kesi

Mahakama Kuu kupitia Mheshimiwa Jaji IGNAS KITUTSI asubuhi ya jana imetupilia mbali maombi madogo ya kesi ya kuomba kupunguziwa gharama za dhamana ya kesi iliyofunguliwa na mwanasiasa Jonas Nkya dhidi ya msanii/mbunge Joseph Haule (Profesa Jay).

Jay

Mahakama imetupilia mbali kesi hiyo na kukubaliana na hoja za mapingamizi ya kisheria yaliyowekwa na jopo la mawakili wa msanii huyo – Tundu Lissu na John Mallya.

Mahakama pia imemuamuru mlalamikaji Jonas Nkya ambaye walikuwa wakigombea pamoja nafasi ya ubunge wa jimbo la Mikumi alipe gharama zote za kesi na usumbufu.

EATV.TV

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364