-->

Mama Ngwea Afunguka Kuhusu Ngwea Kutumia Madawa

Mama mzazi wa msanii Albert Mangwea amezungumzia suala ambalo lilishika vichwa vya habari hususan za burudani kuwa msanii huyo alikuwa anatumia madawa ya kulevya.

ngwea

Akiongea na Planet Bongo ya East Africa Radio, Mama wa Mangwea Bi. Denisia Constantino amesema mwanaye hakuwa mtumiaji wa madawa hayo, kwani yeye kama mzazi alishawahi kumuuliza na kukataa, na kusema iwapo angekuwa mtumiaji angemgundua.

“Kusema kweli mimi naweza nikasema hicho kitu wanachosema wenzake, naweza nikakataa kwa sababu alivyokuwa akija hapa nilikuwa najaribu kuongea naye, kumuelekeza, na kama hayo ni masuala sijui kuhusu dawa, ye alikuwa nasema mama kwa nini mtu ujiumize? Mimi vitu kama hivyo kwa kweli sipo, na ndio maana napenda ku-crush hasa mtu kama anataka kuniongelesha vitu ambavyo haviendani kabisa na utaratibu katika maisha yakwangu, bora nishike ninalojua mwenyewe nafanya nini katika kazi zangu”, alisema mama yake Mangwea Bi. Denisia Constantine.

Pamoja na hayo mama wa msanii huyo amesema kabla hajafariki Ngwea alikuwa akimlalamikia kubaniwa kazi zake, lakini hakuonesha kukata tamaaa.

Eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364