-->

Wolper: Lazima Nimzalie Harmonize

MTOTO wa Kichaga anayetikisa anga la Bongo Muvi, Jacqueline Wolper amenyanyua kinywa chake na kusema; “lazima nimzalie Harmonize (Rajabu Abdulhan, staa wa Bongo Fleva), kwa kuwa nimeridhika naye.”

WOLPER892

Kauli hiyo imekuja zikiwa ni siku chache tangu mwigizaji huyo aamue kuanika uhusiano wake hadharani kupitia mitandao ya kijamii ambapo watu wengi wamekuwa wakimsema vibaya kwamba hayupo ‘serious’ na penzi hilo. Alipoulizwa na mwanahabari wetu kuhusu madongo hayo, alifunguka:

“Hawajui mimi ndiyo nimefika. Kudhihirisha hilo labda niwaambie tu, nampenda kufa na ni lazima nimzalie Harmonize.”

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364